Biblia ni Neno la Mungu. Kwa kuisoma, tunamfahamu Mungu na kupokea uelewa bora wa mpango wake kwa ajili ya maisha yetu. Tumekuchagulia mistari michache kutoka katika Biblia ili kuanza safari yako na Mungu.
Kuna Mungu anayekupenda kwa upendo usioelezeka. Anajua ndani yako kabisa, Yuko pamoja nawe katika nyakati zako za upweke zaidi, na Anakupenda hata katika siku zako mbaya zaidi. Mungu huyu mwenye upendo ni wa kweli, na unaweza kumfahamu. Hataki kingine isipokuwa wewe upate kujionea Upendo Wake binafsi na kugundua kusudi la maisha yako katika uhusiano wako Naye, ukipata utimilifu wa kweli maishani.
Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako kuna furaha tele; Katika mkono wako wa kuume kuna mema mazuri daima. Zaburi 16:11
Nasi tumelijua na kuliamini pendo alilo nalo Mungu kwetu. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. 1 Yohana 4:16
Je, unaamini kwamba Mungu anakufahamu na anakupenda?
Kwa bahati mbaya, hatupati uzoefu wa upendo huu usioelezeka kwa sababu tunampuuza Mungu. Tunatafuta maana, kusudi na utimilifu kila mahali – lakini si kwa Mungu. Tunampuuza na Hatuamini kwamba anataka yaliyo bora kwetu. Kwenda njia yetu wenyewe na matendo ya ubinafsi yanayotokana na maisha haya ndiyo Biblia inayoyaita dhambi. Dhambi hudhuru na kuharibu uhusiano wetu na Mungu, na wengine, na hata na sisi wenyewe. Mwishowe, dhambi inatutenga na kila kitu ambacho Mungu anataka kutupatia, yaani Upendo Wake na maisha yenye kusudi – maisha yanayovuka kifo.
Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake, ili asisikie. Isaya 59:2
Kwa maana wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Warumi 3:23
Unajutia nini zaidi maishani mwako?
Mungu hakututupa. Aliguswa sana na utengano wetu Naye kiasi kwamba Alitukaribia. Alikuja kama binadamu katika Yesu Kristo ili atuonyeshe upendo Wake wa kimbingu katika kila kitu alichosema na kufanya. Mwishowe, hata Alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Alichukua nafasi yetu msalabani, akibeba matokeo yote ya dhambi Yeye mwenyewe. Yesu Alikufa – lakini Alifufuka tena, akashinda kifo na kila kitu kilichotutenganisha na Mungu. Kupitia Yesu tunaweza kuingia katika uhusiano wa kibinafsi na Mungu. Tukiwa na Imani katika Yesu tunaweza kugundua maisha ya upendo, nguvu, na kusudi.
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa. I Petro 3:18
“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16
Yesu ni nani kwako wewe binafsi?
Mungu tayari amefanya kila kitu kutuonyesha jinsi anavyotupenda sana, na ametufungulia njia ya kujionea Upendo Wake. Kupitia Yesu Kristo, anatupa utimilifu na uzima wa milele. Tunaweza kukubali zawadi hii – si kwa jitihada za kibinadamu au matendo mema – bali kwa imani. Tunaanza kwa kusema na Mungu moja kwa moja kupitia maombi. Tunaweza kumwambia kwamba tunajuta kuishi bila Yeye. Na kwamba tunachagua kuishi Naye kuanzia sasa kwa kumwamini Yesu Kristo. Utaamua vipi?
“Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, ili mpate ondoleo la dhambi zenu; nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Matendo ya Mitume 2:38
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Yohana 1:12
Je, ni matokeo gani yangekuwa ikiwa ungeishi kwa ajili ya Mungu kwa kila kitu ulicho nacho na jinsi ulivyo? Ikiwa Yesu angesimama mbele yako sasa hivi na kukuuliza: ‘Je, unataka kuishi nami na kwa ajili yangu?’, jibu lako lingekuwa lipi?
Ikiwa umemwalika Yesu maishani mwako, Muumba wa mbingu na nchi sasa ni Mungu wako binafsi, Mwokozi wako, na rafiki yako. – Hongera kwa uamuzi bora zaidi maishani mwako! Mambo yafuatayo yatakusaidia kufanana zaidi na Yesu.
SOMA
Katika Biblia utamgundua Mungu, mapenzi yake, na jinsi watu walivyoishi na Mungu. Weka mazoea ya kusoma Biblia kila siku. Ikiwa huna Biblia, unaweza kupakua “Bible App” kutoka Lifechurch bure.
Unaweza kusakinisha programu ya Biblia.
OMBA
Unaweza kuongea na Mungu kila mahali na wakati wote kuhusu kila kitu. Mungu ni rafiki yako na anapenda kuwa na mda nawe.
KUTANA
Sasa wewe ni sehemu ya familia ya Mungu pamoja na kila mtu anayemwamini Yeye. Tafuta kanisa au jumuiya ya Kikristo itakayokufanya ujisikie umekaribishwa na mahali ambapo imani yako inaweza kukua.
SHIRIKI
Sasa wewe ni “mwanafunzi” wa Yesu. Waambie wengine yale unayojionea na Mungu maishani mwako na kile Yesu alichowafanyia (kwa kutumia THE FOUR).
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17
Nao walidumu katika mafundisho ya mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Matendo ya Mitume 2:42
You will be redirected to your country's page...